26. Ni ipi hukumu ya kula na kunywa kwa kudhania kuwa bado ni usiku au kukata swawm kwa kudhania kuwa jua limeshazama?

Swali 26: Ni ipi hukumu ya kula na kunywa kwa kudhania kuwa bado ni usiku au kukata swawm kwa kudhania kuwa jua lishazama?

Jibu: Akila na kunywa huku akiwa na shaka kama alfajiri imeshaingia, swawm yake ni sahihi. Hahitajii kuilipa siku hii. Ama ikimbainikia kuwa alikula au kunywa baada ya alfajiri kuwa wazi mbali na mashaka yote, ni lazima kwake kulipa. Hali kadhalika ikiwa alikata swawm kwa kudhania kuwa jua limeshazama. Ikimbainikia kuwa bado halijazama basi inamlazimu kuilipa siku hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 12/06/2017