Swali 26: Ni ipi hukumu ya ambaye aliyazuia matapishi ilihali amefunga? Je, ailipe siku hiyo au hapanaa?

Jibu: Hukumu yake ni kuwa si lazima kulipa. Ama akijitapikisha ni lazima kulipa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na ambaye atajitapisha basi ni lazima kwake kulipa.”

Ameipokea Imaam Ahmad na waandishi wa ”as-Sunan” wane kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 29
  • Imechapishwa: 10/05/2019