Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

21- Kama ambavyo anazingatiwa ni Mwenye kuwahuisha wafu na amestahiki jina hili kabla ya kuwapa uhai, kadhalika amestahiki jina la Muumbaji kabla ya kuwaumba.

MAELEZO

Yeye (Subhaanah) ni Mwenye kusifiwa kwamba ni Mwenye kuwahuisha wafu milele. Sifa hii si yenye kukosekana mpaka awahuishe waliokufa kikweli. Uhakika wa mambo ni kwamba daima alikuwa na sifa hii. Ama wakati atakapowapa uhai wafu inahusiana na kitendo chenye kujijadidi. Yeye (Subhaanah) anahuisha na kufisha pale anapotaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 44
  • Imechapishwa: 19/09/2019