26. Mwenye busara na udugu III


1- Mwenye busara hamuabishi nduguye kwa ajili ya kosa lake. Wana maumbile ya kufanana. Bali anatakiwa kufutilia mbali na nduguze.

2- Aliye na busara anatakiwa kuhakikisha kuwa si mwenye kuwaonea hasadi nduguze. Kuwa na hasadi kwa marafiki ni katika maradhi ya mapenzi kama ambavyo ukarimu katika mapenzi ni katika sampuli kubwa ya utoaji. Kwa kuwa mapenzi ya kweli hayawezi kutoka kwenye moyo uliyo na maradhi. Mtu anatakiwa kuchunga asimuudhi ndugu yake. Mwenye kuonekana kuwa ni mwenye kuudhi kwa rafiki yake ni mwenye kujisalimisha kwa adui yake.

3- Miongoni mwa mambo makubwa yanayomliwaza mtu wakati wa maudhi ni kuridhia makadirio na kukutana na ndugu.

4- Ibraahiym bin ´Abdillaah al-´Adaniy amesema:

“Sufyaan aliulizwa kuhusu maji ya maisha. Akasema: “Ni kukutana na ndugu.”

5- Sufyaan amesema:

“Inawezekana nilikutana na mmoja katika ndugu na nikawa ni mwenye uelewa mwezi mmoja baada ya kuonana naye.”

6- Abu Sulaymaan amesema:

“Nilimtazama mmoja katika ndugu zetu wa ´Iraaq na nikatendea kazi yale niliyoyaona kwa muda wa mwezi mmoja.”

7- Rabi´ah amesema:

“Murua imegawanyika aina mbili; murua wa kusafiri na murua wa kuwa nyumbani. Murua wa safarini ni kusimamia gharama za wengine, kutokuwa na tofauti na marafiki zako na kutania sana pasi na kumkasirisha Allaah. Murua wa kuwa nyumbani ni siku zote kuwa msikitini, kuwa na marafiki wengi kwa ajili ya Allaah na kusoma Qur-aan.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 93-95
  • Imechapishwa: 14/02/2018