26. Maswahabah hawakutofautiana katika ´Aqiydah


Maswahabah hawakutofautiana katika suala hili. Ahl-ul-Ahwaa´ wanaeneza tofauti katika mambo ya misingi na matawi na kusema kuwa Maswahabah walitofautiana katika ´Aqiydah. Ni uongo. Hawakutofautiana. Upande mmoja ´Aaishah anakanusha kuwa Kuonekana kulipitika kwa macho. Upande mwingine Ibn ´Abbaas anathibitisha kuwa Kuonekana kulipitika, lakini hata hivyo kwa moyo. Tofauti iko wapi? Hakuna.

Imaam Ahmad amesema:

“Tunaiamini Hadiyth hii kama ilivyo kama jinsi ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Mtu anaweza kufahamu kuwa anaonelea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola Wake kwa macho kutokana na upokezi wa Ibn ´Abbaas. Hivi sasa mmejua namna ambavyo inatakiwa kukabiliwa na kwamba Hadiyth hiyo sio Swahiyh. Maneno yake yasiyofungamana yanatakiwa kufasiriwa kwa maneno yake yaliyofungamana. Kwa njia hiyo natija inayopatikana ni kwamba Maswahabah hawakutofautiana katika suala hili. Hata hivyo kuna wanachuoni waliokuja nyuma ambao wameathirika na maneno ya Ahmad na kuamini kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola Wake kwa macho yake. Pamoja na hivyo ufahamu wao huu ni wa makosa kwa sababu Ahmad pia amezungumzia suala hili kwa njia ya kufungamanishwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 390
  • Imechapishwa: 21/08/2017