26. Kumfunza mtoto Qur-aan kunazima hasira za Allaah

… na kufanyiwa kazi na viungo vyao vya miili – Kwanza moyo ndio huanza kutenda kisha unafuatiwa na viungo vya mwili. Matendo yamegawanyika sampuli mbili:

1- Matendo ya mioyo. Kwa mfano kumcha Allaah, kumukhofu, kuwa na matumani Kwake na kumpenda Allaah.

2- Matendo ya viungo vya mwili ni yenye kufuatiwa na matendo ya mioyo. Kwa mfano swalah, kufunga, kuhiji na jihaad.

Kwani hakika inasemekana kwamba imepokelewa kuwa kumfunza mtoto mdogo Kitabu cha Allaah kunazima ghadhabu za Allaah… – Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba kumfunza mtoto mdogo Kitabu cha Allaah kunazima ghadhabu za Allaah[1]. Neno inasemekana kuwa imepokelewa (روي) inafahamisha juu ya udhaifu. Kwa hiyo ni Hadiyth dhaifu. Lakini hata hivyo maana yake ni sahihi. Allaah anafurahi watoto wadogo wakafunzwa Qur-aan. Huu ni utangulizi wa malezi bora. Ndani yake kuna kanuni za malezi bora na sio malezi ya wamagharibi ambayo yanapigiwa debe na wakomunisti hii leo.

[1] Sikuipata katika vitabu na marejeo ya Hadiyth zinavyozingatiwa ipo katika ”Musnad” ya ar-Rabiy´ (25) ambayo ina majanga mengi. Yanafahamika maneno ya wanachuoni juu yake. Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) hapa ameitaja kwa namna ya inasemekana kuwa imepokelewa (روي), kana kwamba haikuthibiti kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 26
  • Imechapishwa: 13/07/2021