26. Du´aa ya mvua


124- Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Wanawake wanaolia walikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema:

اللَّهُمَّ اسْقِنَا غَيْثاً مُغِيثاً مَرِيئاً مَرِيعاً نَافِعاً غير ضارٍّ عاجلاً غير آجِلٍ

“Ee Allaah! Tunyeshelezee mvua yenye kuokoa, yenye kustawisha, yenye rutuba na isiyodhuru, sasa hivi na isiyochelewa.”

125- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) amesema:

“Watu walilalamika kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na ukame wa mvua. Akaamrisha kuletwe minbari. Ikawekwa mahala pa kuswalia. Akawaahidi watu siku moja watoke nje. Wakati jua lilipochomoza akatoka Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nje, akapanda juu ya minbari, akasema “Allaahu Akbar” na akamhimidi Allaah (´Azza wa Jalla). Kisha akasema: “Mmelalamika kuwa ardhi zenu zimekauka na kwamba hampati mvua yoyote. Allaah (Subhaanah) amewaamrisha kumuomba na akaahidi kuwaitikia.” Kisha akasema:

الْحَمْدُ للهِ رَبِّ الْعَالمِينَ الرَّحْمنِ الرَّحيمِ مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ لا إِلهَ إِلاَّ الله يَفْعَلُ ما يُرِيدُ اللهُمَّ أَنتَ الله لا إِله إِلا أَنْتَ أَنْتَ الغَنِيُّ وَنَحْنُ الْفُقَرَاءُ أَنْزِلْ عَلَيْنَا الغَيْثَ واجْعَلْ مَا أَنْزَلْتَ لَنَا قُوَّةً وَبَلاغاً إِلى حينٍ

“Himdi zote ni Zake Allaah, Mola wa walimwengu, Mwingi wa kurahamu, Mwenye kurahamu, Mfalme wa siku ya Qiyaamah! Hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Anafanya alitakalo. Ee Allaah! Wewe ndiye Allaah na hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe. Wewe ndiye Tajiri na sisi ni mafukara. Tuteremshie mvua na jaalia kile unachotuteremshia kuwa ni nguvu na huru huko mbeleni.”

Kisha akanyanyua mikono mpaka ikaweza kuonekana makwapa yake. Halafu akawazungukia watu na kuwapa mgongo wake na kuzunguka kwenda ndani na nje kwenye nguo yake ambayo ilikuwa imefunika mwili wake. Mikono yake ilikuwa bado iko juu. Kisha akawageukia watu, akateremka na kuswali Rakaa mbili. Allaah (´Azza wa Jalla) akaleta mawingu. Kukaanza kupiga radi na kwa idhini ya Allaah (Ta´ala) kukaanza kunyesha. Hakuwahi kufika kwenye Msikitini wake kabla ya kuanza kutiririka maji. Alipoona haraka waliokuwa nayo ya kuchukua kinga akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na akasema: “Ninashuhudia kwamba Allaah juu ya kila jambo ni Muweza na kuwa mimi ni mja Wake na ni Mtume Wake.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 84-86
  • Imechapishwa: 21/03/2017