26. Dalili ya kwamba Allaah ndio Mola wa walimwengu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

 الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Mola wa  walimwengu.”  (al-Faatihah 01 : 02)

MAELEZO

Ili kuthibitisha ya kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mlezi wa viumbe wote, mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ametumia dalili maneno Yake (Ta´ala):

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Mola wa  walimwengu.”

Hapa kuna sifa ya ukamilifu, utukufu na ukubwa juu ya Allaah (Ta´ala) pekee.

رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Mola wa  walimwengu.”

Bi maana Yule aliyewalea kwa neema, amewaumba, amewamiliki na kuyaendesha mambo yao kama anavyotaka (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 46
  • Imechapishwa: 20/05/2020