26- Hamdayn bin Ahmad Hamdayn ametuhadithia: Haaruun bin Ahmad ametuhadithia: Abuu Khaliyfah ametuhadithia: Musaddad ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Yuunus, Hishaam na al-Mu´allaa, kutoka kwa al-Hasan aliyeeleza kuwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Du´aa ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikithirisha kuiomba ni:

يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ

“Ee Mwenye kuzigeuza nyoyo! Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nakuona kuwa unaomba du´aa hii mara nyingi.” Akasema: “Hakuna mwanaadamu yeyote isipokuwa moyo wake uko baina ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall). Akitaka kuunyoosha, anaunyoosha, na akitaka kuupindisha, anaupindisha.”[1]

[1] Ahmad (6/91), an-Nasaa’iy (16059) na Ibn Abiy ´Aaswim (224). ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy amesema:

”Shaykh al-Albaaniy ameashiria kuwa Hadiyth ni Swahiyh kupitia mapokezi aminifu.” (al-Arba´uun fiy Dalaa’il-it-Tawhiyd, uk. 75)

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 56
  • Imechapishwa: 02/02/2017