26 Dalili ya ishirini na nne kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

24- Abul-Qaasim Yahyaa bin As´ad bin Buush ametuhadithia: Abul-´Izz Ahmad bin ´Ubaydillaah bin Kaadis ametuhadithia: Abu ´Aliy Muhammad bin al-Husayn al-Jaaziriy ametuhadithia: Abul-Faraj al-Mu´aafaa bin Zakariyyaa al-Jariyriy ametuhadithia: Muhammad bin al-Qaasim al-Anbaariy ametuhadithia: Muhammad bin al-Marzabaan ametuhadithia: Abu ´Abdir-Rahmaan al-Jawhariy ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin adh-Dhwahhaak ametuhadithia: al-Haytham bin ´Adiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Awaanah bin al-Hakam aliyesema:

“Wakati ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz alipokuwa khalifah kundi la wanashairi walikuja kwake. Wakasimama nje ya mlango wake kwa masiku kadhaa pasi na kupewa idhini. Siku moja wakati walipokuwa katika hali hiyo na wameazimia kurudi. Ndipo ´Adiy bin Artwa’ah akapita karibu yao ambapo Jariyr akamwambia:

Ee mpandaji unayeendesha kipando chako

huu ni wakati wako – mimi wakati wangu umeshapita

Msalimie khalifa wetu ukikutana naye

kwamba nimekuwa kama mfungwa karibu na mlango

Usizisahau haja zetu – naomba usamehewe

nimekuwa mbali na familia yangu na nchi yangu kwa muda mrefu

´Adiy akaenda kwa ´Umar na kusema: “Ee kiongozi wa waumini! Wanashairi wako nje ya mlango wako. Mishale yao ina sumu na maneno yao ni yenye kukubalika.” Akasema: “Ole wako, ee ´Adiy! Mimi ninahusiana nini na wanashairi?” Akasema: “Allaah amtie nguvu kiongozi wa waumini! Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposifiwa alitoa. Hakika una kiigizo chema kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Akasema: “Vipi yaani?” ´Adiy akasema: “al-´Abbaas bin Mirdaas as-Sulamiy alimsifu ambapo akampa koti. “ ´Umar akauliza: “Unaweza kuelezea chochote katika yale aliyosema?” Akajibu: “Ndio:

Nimekuona, ee kiumbe bora kabisa

eneza na funza Kitabu kilichokuja kwa haki

Umetuwekea katika Shari´ah dini ya mwongozo

baada ya kuwa wapotofu na wenye giza kunako haki

Umekiangazia kitu kilicho na ukungu kwa dalili

na umezima moto uwakao

Ni nani awezaye kunifikishia salamu kwa Mtume Muhammad

kila mmoja atalipwa kwa kile alichotanguliza

Umeinyoosha njia ya haki baada ya kupinda kwake

Nguzo yake ilikuwa imebomoka tokea hapo kitambo

Ametakasika Mola wetu aliye juu ya ´Arshi

Nafasi ya Allaah iko juu na ni kubwa[1]

Kisha akataja yaliyobaki.

[1] Ibn ´Abdi Rabbih al-Andalusiy katika ”al-´Aqd al-Fariyd” (1/205). adh-Dhahabiy amesema:

”al-Haytham bin ´Adiy ni dhaifu.” (al-´Uluww, uk. 42)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 106-108
  • Imechapishwa: 07/06/2018