26. Dalili juu ya mkono wa Allaah 12

26- Ahmad bin Muhammad bin Sa´iyd ametuhadithia: Ya´quub bin Yuusuf bin Ziyaad ametuhadithia: ´Ubayd bin Sulaymaan as-Samiyn ametuhadithia: Mu´ammar bin Zaa-idah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:

“Kuna mwanachuoni wa kiyahudi alienda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Abul-Qaasim! Je, imekufikia kwamba Allaah (´Azza wa Jall) atawabeba viumbe kwenye kidole, mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, miti kwenye kidole na ardhi kwenye kidole?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na Allaah akateremsha:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]

´Iysaa bin Yuunus na Qays bin ar-Raabiy´ vilevile wameipokea kwa mlolongo wa wapokezi huu kutoka kwa al-A´mash.

[1] 39:67

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 62-63
  • Imechapishwa: 28/02/2018