26. Bora ni yeye kuswali nyumbani kwake


Swali 26: Ni lipi bora zaidi kwa mwanamke katika nyusiku za Ramadhaan aswali nyumbani kwake au aswali msikitini na khaswa kukiwa kuna mawaidha na ukumbusho? Ni zipi nasaha zako juu ya wanawake wanaoswali misikitini?

Jibu: Bora ni yeye kuswali nyumbani kwake. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nyumba zao ni bora kwao.”

Isitoshe kitendo cha wanawake kutoka nje mara nyingi hakisalimiki na fitina. Kwa hivyo mwanamke kubaki nyumbani kwake ni bora kuliko kutoka kwenda kuswali msikitini. Mawaidha na ukumbusho yanaweza kumfikia kwa njia ya kanda.

Nasaha zangu kwa wale wanaoswali msikitini ni kwamba watoke majumbani mwao pasi na kuonyesha mapambo wala kujitia manukato.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 23
  • Imechapishwa: 24/07/2021