26. Allaah amekizunguka kila kitu kwa ujuzi


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

Anayajua ya siri na yaliyofichikana na amelingana juu ya ´Arshi. Elimu Yake iko kila mahali na haikosekani mahali kote.

MAELEZO

Kule kuyajua Kwake yaliyomo mbinguni na ardhini na yaliyomo chini ya ardhi hayapingani na kuwa Kwake juu ya ´Arshi. Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) amekizunguka kila kitu na hafichikani na kitu (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 61
  • Imechapishwa: 08/01/2018