Swali 25: Baadhi ya wagonjwa wa Kiislamu wanakufa kinyume na Qiblah kwa sababu vitanda mahospitali vimewekwa kinyume na Qiblah.

Jibu: Hakuna neno katika hilo. Sunnah ni kumwelekeza mgonjwa Qiblah wakati wa kutaka kufa kukiwa kuna wepesi wa kufanya hivo. Vinginevyo hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 48
  • Imechapishwa: 11/10/2019