25. Upetukaji wa ´Iyd ´Abbaasiy juu ya madhehebu

Wakati fulani huenda baadhi yao wakatumbukia katika uchupaji. Kwa mfano ´Iyd ´Abbaasiy amesema:

“Kwa mujibu wao wanaona kuwa mwanachuoni ni yule mwenye kufahamu na kuhifadhi  vitabu vya Fiqh katika madhehebu. Hivyo basi wanamwacha ahukumu na atoe fatwa. Bali kupitia vitabu hivi wanamhalalishia damu, tupu na mali.”[1]

Jambo la kwanza vitabu vya Fiqh viko na elimu. Mwanachuoni wa kweli ni yule mwenye kufahamu kila maoni kwa dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Kwa ajili hii wameifasiri Fiqh kwamba maana yake ni kuzitambua hukumu za Kishari´ah kwa dalili zake zilizopambanuliwa. Ama kuhusu anayejua hukumu ya madhehebu fulani pasi na kujua dalili zake basi elim yake ni pungufu.

Jambo la pili ni kwamba hapana shaka kuwa vitabu vya Fiqh vimejengea baadhi ya hukumu juu ya Hadiyth dhaifu.

Jambo la tatu yale yanayohalalisha damu, tupu na mali ni yenye kutoka katika dalili sahihi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kwa sababu imamu wa madhehebu ni Muhaddith mkubwa.

Jambo la nne ni kwamba tofauti inaweza kupatikana kupitia utumiaji wa dalili kutokana na kwamba imefahamika kwa njia nyingi. Ndipo wanachuoni wakatofautiana.

Jambo la tano kosa linaweza kupatikana katika madhehebu kwa sababu ya Ijtihaad.

Jambo la sita mwandishi huyu hawezi kuleta hukumu hata moja ambayo madhehebu yamehukumu kuua nafsi, kusimamisha adhabu au kupora mali kwa kutegemea Hadiyth dhaifu ambayo inatakiwa kutupiliwa mbali. Ilikuwa ni aula zaidi kwake kutochupa mipaka namna hii jambo ambalo limepelekea kukosolewa.

Jambo la saba ni kwamba kupatikana kitu kama hichi haina maana kwamba wana nia mbaya dhidi ya Saudi Arabia au kwamba wanakusudia kuitokomeza. Huu ni ukosoaji wa kielimu ambao haupelekei katika khatari yoyote ya kisiasa.

[1] Bid´at-ut-Ta´assub al-Madhhabiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 04/12/2018