25. Uharamu wa kuelezea siri za chumbani


23- Uharamu wa kueneza siri za chumbani

Ni haramu kwa kila mmoja katika wao kueneza siri zinazohusiana na mambo ya chumbani. Kuna Hadiyth mbili juu ya hilo:

1- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika watu waovu kabisa mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah ni mwanamume anayemwingilia mkewe na yeye akamwingilia kisha akaeneza siri zake.”[1]

2- Asmaa´ bint Yaziyd amesimulia ya kwamba alikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) wakati ambapo wanaume na wanawake walikuwa wameketi ambapo akasema:

“Huenda mwanaume akasema yale aliyofanya na mkewe na huenda mwanamke akasema yale aliyofanya na mumewe?” Wakanyamaza na hawakujibu kitu. Nikasema: “Ninaapa kwa Allaah! Wanawake hufanya na wanaume hufanya.” Akasema: “Msifanye hivo! Hivyo ni kama mfano wa shaytwaan wa kiume aliyekutana na shaytwaan wa kike njiani akamwingilia na huku watu wanatazama.”[2]

[1] Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (01/67/07) na Muslim katika njia moja wapo (04/157), Ahmad (03/69), Abu Nu´aym (10-236-237), Ibn as-Sunniy (608), al-Bayhaqiy (608), al-Bayhaqiy (07-193-194) kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy.

[2] Ameipokea Ahmad na ina shawahidi kupitia Hadiyth ya Abu Hurayrah kwa Ibn Abiy Shaybah, Abu Daawuud (01/339), al-Bayhaqiy, Ibn as-Sunniy nambari (609). Dalili ya pili ameipokea al-Bazzaar kupitia kwa Sa´iyd nambari (1450) – Kashf-ul-Astaar. Dalili ya tatu ameipokea Salmaan katika “al-Hilyah” (01/186).

Hadiyth kwa shawahidi hizi ni Swahiyh au angalau kwa uchache ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 139-141
  • Imechapishwa: 19/03/2018