140- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Ee Bilaa, toa na wala usiogope kupungukiwa kwa Mola wa waumini.”[1]

141- Wanachuoni wanasema kuwa khofu kama hiyo ni kumdhania vibaya Allaah na kumdhania Allaah vibaya ni kufuru. Hilo ni kwa sababu Allaah amemuahidi yule mwenye kutoa kumpa kingine hapa duniani na thawabu huko Aakhirah. Allaah amesema juu ya kitu kingine:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ

“Na chochote mtoacho katika kitu, basi Yeye Atakilipa, Naye ni Mbora wa wenye kuruzuku.” (34:39)

Amesema juu ya thawabu:

يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ

“Allaah Humzidishia Amtakaye.” (02:261)

Asiyetoa swadaqah kwa ajili ya kuogopa kupungukiwa na kuogopa ufakiri anakumbushia asiyeamini maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

142- Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ni ugonjwa upi mabaya kama ubakhili?”[2]

143- Ilipokuwa ubakhili unamnyima mtu kupewa kingine hapa duniani , thawabu huko Aakhirah na kumdhania vibaya Allaah, ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaomba kinga nao aliposema:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba unikinge na hamu na huzuni, kushindwa na uzembe, ubakhili na woga, fujo za deni na kushinda kwa wanaume.”[3]

Kuogopa kupungukiwa kunaondoka kwa njia mbili:

1- Kumdhania vyema Allaah (´Azza wa Jall) na kujua kuwa Ataleta kingine. Hakika Mola wangu ni mwaminifu na mkarimu:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ

“Na chochote mtoacho katika kitu, basi Yeye Atakilipa, Naye ni Mbora wa wenye kuruzuku.”

2- Kuwa mwanaume wa kisawasawa ambaye hutaki kitu kingine zaidi ya chenye kutosheleza. Mtu kama huyu anatoa pindi kuna uzito na urahisi. Haogopa kupungukiwa. Fikira zake ziko mbali kabisa na hayo. Mwenye choyo tu ndiye huogopa upungukiwaji.

144- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa kulia wa Allaah umejaa. Haupungui kwa kutoa mchana na usiku. Je, hamuoni vile Alivyotoa tangu Alipoumba mbingu na ardhi pasi na chochote kilichomo katika mkono Wake wa kulia kupungua?”[4]

[1] Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (2661).

[2] al-Bukhaariy (6/237).

[3] al-Bukhaariy (6363).

[4] al-Bukhaariy (4683) na Muslim (993).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 18/03/2017