25. Tahadhari juu ya makundi yenye utata na mashaka

Makundi haya ya Kiislamu ambayo misingi yake imesimama mbali na Qur-aan na Sunnah ukweli wa mambo ni kuleta mpasuko kwa waislamu na shari na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko kheri zake. Pindi yalipochagua njia isiyoishilia katika Qur-aan na Sunnah na hawapakui kutoka kwa Salaf wa Ummah huu, ndipo wakaingiliwa na kasoro kupitia mlango huu.

Kwa hiyo ala ala tahadharini na makundi haya yenye utata. Vijana! Msiwe ni vichinjwa vya fikira zao. Naapa kwa Allaah kwamba makundi hayo hayajaingia ndani ya mji na yakapuliza sumu yazo isipokuwa kati yao huenea mpasuko na tofauti na kudhihiri chuki na bughudha baina ya watoto wake. Kama unataka dalili juu ya hilo linganisha kati ya hali yetu wakati tulipokuwa juu ya mfumo wa Shaykh na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na hali yetu hii leo. Makundi haya yametenganisha kati ya wanachuoni na vijana na yameweka baina yao kizuizi.

Hapo kabla tulikuwa ni wenye kuwaamini wanachuoni wetu uaminifu mkubwa na tukichukua elimu kutoka kwao. Athari katika hali hiyo ilikuwa ni yenye kutofautiana na athari ya hali ambayo nimeiashiria punde kidogo. Kipindi cha hali ya kwanza tulikuwa juu ya kheri na uongofu. Ama hali yetu hivi sasa ni ya vurugu, usumbufu na mfano wa hayo.

Jengine ni kwamba makundi haya yameziharibu fikira za baadhi ya vijana wetu na yakawachafulia sura ya mfumo. Aidha yamefanikiwa kufanya wawe ni wenye kupenda na kuchukia kwa ajili yao peke yake.

Miongoni mwa mambo yasiyokuwa na shaka ni kwamba makundi haya yatawatumia wafuasi wake walioghurika kuleta mapinduzi au kuingia ndani ya fitina. Ee kijana! Usisahau tukio lilitokea msikiti Mtakatifu!

Tunamuomba Allaah awaepushe waislamu yote yenye kuchukiza na atulinde sote na majanga yote.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 15/10/2020