25. Qiblah kugeuzwa na swawm kufaradhishwa


Mwaka huohuo katika Sha´baan Qiblah kikabadilishwa kutoka Yeruselamu kwenda Ka´bah. Hayo yalipitika miezi kumi na sita tangu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika al-Madiynah. Imesemekana vilevile kwamba ni miezi kumi na saba. Yote mawili yamepokelewa katika al-Bukhaariy na Muslim.

Mtu wa kwanza kuelekea Ka´bah alikuwa ni Abu Sa´iyd bin al-Mu´allaa na rafiki yake, kama alivyopokea an-Nasaa´iy:

”Tulimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anawakhutubia watu na anawasomea kuhusu kugeuzwa kwa Qiblah. Nikamwambia rafiki yangu: ”Hebu njoo tuswali Rakaa´ mbili sisi tuwe wa mwanzo kuswali kuelekea Ka´bah.” Tukaenda na tukajificha na kuswali kukielekea. Kisha akashuka Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawaswalisha watu Dhuhr.”

Kadhalika ikafaradhishwa swawm ya Ramadhaan  na siku ya kufuata ikafaradhishwa Zakaat-ul-Fitwr.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 45
  • Imechapishwa: 26/04/2018