25. Mke anatakiwa kuhifadhi nyumba ya mume wake

Miongoni mwa haki za mume juu ya mke wake ni yeye kuihifadhi nyumba yake na asimwache akaingia yeyote asiyetaka aingie. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haki zenu juu yao ni wao kutomwacha yeyote yule mnayemchukia akalala kwenye vitanda vyenu.”[1]

Amesema vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ama kuhusu haki zenu juu ya wake zenu, wasimwache yeyote yule mnayemchukia akalala kwenye vitanda vyenu wala kuingia katika nyumba zenu.”[2]

[1] Muslim (1218).

[2] at-Tirmidhiy (1163) na Ibn Maajah (1851). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa at-Tirmidhiy.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 39
  • Imechapishwa: 24/03/2017