25. Mambo ambayo wanapswa kufunzwa

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

… na kufanyiwa kazi na viungo vyao vya miili. Kwani hakika inasemekana kwamba imepokelewa kuwa kumfunza mtoto mdogo Kitabu cha Allaah kunazima ghadhabu za Allaah na kwamba kujifunza kitu udogoni ni kama kuchonga kwenye jiwe.

MAELEZO

Watoto wanatakiwa kufunzwa yale ambayo nyoyo zao zinapasa kuyaamini katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah iliyojengeka juu ya Qur-aan na Sunnah. Hawatakiwi kufunzwa maoni ya watu, mantiki, falsafa na upumbavu. Mafunzo yanakuwa kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah, kitu ambacho ni chepesi kwa idhini ya Allaah. Isitoshe ndani yake mna nuru, baraka na kheri. Kuhusu mantiki na mijadala ni mambo yanazifanya nyoyo kuwa na giza. Wale ambao walibobea katika mambo hayo hawakufikia kheri yoyote. Bali ni kwamba mwishoni mwa uhai wao walitamani lau wasingejishughulisha nazo na kwamba laiti wangechukua elimu ya Salaf. Haya yametajwa katika historia na maisha yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 13/07/2021