Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kutaka msaada ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

”Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” (al-Faatihah 01 : 05)

Katika Hadiyth pia imekuja:

“Unapotaka msaada, basi mtake msaada Allaah.”[1]

MAELEZO

Vilevile kutaka msaada ni ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunakuabudu na Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.” (01:05)

Katika Hadiyth pia imekuja:

“Unapotaka msaada, basi mtake msaada Allaah.”

Mja anatakiwa kumtaka msaada Allaah na kumfanya umkumbuke, kumshukuru, kukutii na kufanya kila lililo na kheri. Mtake msaada Allaah katika kila la muhimu.

[1] Ahmad (1/307) na at-Tirmidhiy (2516) aliyesema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 26/12/2016