Swali 25: Je, inafaa kusoma Qur-aan katika ijumaa kwa sauti ya juu msikitini[1]?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kupaza sauti yake kwa kisomo au kitu kingine ndani ya msikiti akiwa anawashawishi waswaliji au wasomaji walioko pambizoni mwake. Sunnah ni yeye kusoma kisomo ambacho hakiwaudhi wengineo. Kutokana na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba siku moja aliwatokezea watu msikitini na wao huku baadhi wananyanyua sauti zao juu ya wengine kwa kisomo ambapo akasema:

“Enyi watu! Kila mmoja wenu anamnong´oneza Mola Wake. Hivyo baadhi wasisome kwa sauti ya juu kwa wengine.” Au alisema: “Hivyo baadhi wasipaze sauti zao juu ya wengine.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/392-393).

[2] Imaam Ahmad (4692, 5096) na Maalik katika ”al-Muwattwa´” (163).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 66
  • Imechapishwa: 29/11/2021