25. Damu inayokatika siku moja-mbili baadaye ikarudi


Swali 25: Baadhi ya wanawake damu inaendelea kuwatoka na mara nyingine inakatika kwa muda wa siku moja au mbili kisha inarudi. Ni ipi hukumu katika hali hii kwa nisba ya funga, swalah na ´ibaadah nyenginezo?

Jibu: Kinachotambulika kwa wanachuoni ni kwamba mwanamke akiwa na ada ambapo eda yake ikamalizika basi atatakiwa kuoga, kuswali na kufunga. Kile anachoona baada ya siku mbili au tatu sio hedhi. Kwa sababu kwa mujibu wa wanachuoni hawa muda wa hedhi wa chini kabisa ni siku kumi na tatu. Wanachuoni wengine wamesema kuwa muda wa kuwa ataona damu basi ni hedhi na muda wa kuwa atatwahirika kutokamana nayo basi atazingatiwa ni msafi hata kama hakuna masiku kumi na tatu kati ya hedhi mbili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 22
  • Imechapishwa: 17/07/2021