25. Dalili ya kwamba swadaqah huanguka kwenye mkono wa Allaah

25- Twaahir bin Muhammad bin ´Aliy ametuhadithia: Haamid bin Muhammad ametuhadithia: ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Abuu Nu´aym ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah: as-Saa-ib ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiy Qataadah al-Muhaaribiy: Nilimsikia ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) akisema:

“Swadaqah huanguka mkononi mwa Allaah (´Azza wa Jall) kabla ya kuanguka mikononi mwa yule mwombaji.”

28- Kisha akasoma ´Abdullaah al-Ja´fiy: Swaalih bin Waswiyf al-Kinaaniy ametuhadithia: Ahmad bin Mulaa´ib ametuhadithia: ´Abdus-Swamad (bin an-Nu´maan) ametuhadithia: ´Abdul-Malik bin al-Husayn ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim bin ´Ubaydillaah, kutoka kwa Qaasim bin Muhammad, kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema mfano wa hivo[1].

[1] ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy amesema:

”al-Haythamiy ameitaja katika ”az-Zawaa-id” na amesema: ”Imepokelewa na al-Bazzaar na wapokezi wake ni waaminifu.” (Majma´-uz-Zawaa-id (3/112)) (al-Arba´uun fiy Dalaa’il-it-Tawhiyd, uk. 74)

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 55
  • Imechapishwa: 31/01/2017