25. Dalili ya ishirini na tatu kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


23- Nilimsomea Abul-Ma´aaliy ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin Ahmad bin Swaabir as-Sulamiy: ash-Shariyf Abul-Qaasim al-Husayniy amekukhabarisheni: ´Abdul-´Aziyz bin Ahmad al-Kitaaniy ametuhadithia: Abu Muhammad ´Abdur-Rahmaan bin ´Uthmaan ametuhadithia: Ami yangu Muhammad bin al-Qaasim bin Ma´ruuf ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin Sa´iyd ametuhadithia: Abu Bakr bin Abiy Shaybah ametuhadithia: ´Abdah bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Abu Hayyaan, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit aliyesimulia kwamba Hassaan bin Thaabit alimsomea mashairi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Kwa idhini ya Allaah nashuhudia ya kwamba Muhammad

ni Mtume wa Yule ambaye Yuko juu ya mbingu

Na kwamba baba yake na Yahyaa na Yahyaa wote wawili

na matendo yenye kukubalika kwa Mola wake

Na kwamba mwana wa Maryam ambaye ni adui wa mayahudi

ni Mtume, aliyetumwa na Yule ambaye anamiliki ´Arshi

Pindi ndugu wa vilima vya mchanga atapojitokeza kati yao

atapambana kwa ajili ya Allaah na atafanya uadilifu[1].

[1] Ibn Abiy Shaybah (8/695). adh-Dhahabiy amesema:

“Cheni ya wapokezi si timilifu.” (al-´Uluww, uk. 40)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 106
  • Imechapishwa: 07/06/2018