25. Dalili juu ya mkono wa Allaah 11

25- Muhammad bin Sahl bin al-Fudhwayl al-Kaatib ametuhadithia: ´Aliy bin Harb ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah na Muhammad bin Fudhwayl ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:

“Kuna mwanamume alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Abul-Qaasim! Je, imekufikia kwamba Allaah (´Azza wa Jall) atawabeba viumbe kwenye kidole, mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, miti kwenye kidole na ardhi kwenye kidole?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na Allaah akateremsha:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]

[1] 39:67

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 27/02/2018