25. Aina ya pili majina ya haramu


2- Majina ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Haijuzu kutoa jina kwa jina ambalo ni maalum kwa Mola (Subhaanahu wa Ta´ala). Mfano wa majina hayo ni ar-Rahmaan, ar-Rahiym, al-Khaaliq na al-Baariy. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadilisha majina ya sampuli hiyo.

Katika Qur-aan tukufu:

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua mwengine mwenye Jina kama Lake?” (19:65)

Bi maana hana anayefanana Naye anayestahiki mfano wa jina Lake kama ar-Rahmaan[1].

[1] Tazama “al-Jaami´ li Ahkaam-il-Qur-aan” (11/130) ya al-Qurtwubiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 22
  • Imechapishwa: 18/03/2017