Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

MAELEZO

Msingi wa tatu ni mtu kumjua Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili linapatikana kwa mtu kusoma maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ´ibaadah zake, tabia, kulingania katika dini ya Allaah  (´Azza wa Jall), kupambana kwake jihaad katika njia Yake na mengineyo. Kwa ajili hii inampasa kila mtu ambaye anataka kuzidisha maarifa juu ya Mtume wake na imani yenye nguvu, basi asome historia yake kiasi atakavyoweza. Kisomo kihusiane na hali yake katika vita na usalama, kipindi chake cha matatizo na kipindi chake cha raha na hali zake zingine zote.

Tunamuomba Allaah (´Azza wa Jall) atujaalie katika wale wenye kumfuata Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa ndani na kwa nje na atufishe katika hali hiyo – hakika Yeye ni muweza wa hilo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 45
  • Imechapishwa: 20/05/2020