24. Sharti ya nne na ya tano ya Shahaadah: Unyenyekevu na ukweli

4- Sharti ya nne: Unyenyekevu. Mtu anatakiwa anyenyekee yale yanayofahamishwa nalo. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ

“Anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mfanya ihsaan, basi kwa hakika ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika.”[1]

Kishikilio madhubuti ndio “Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Maana ya:

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ

“Anayeusalimisha uso wake… “

bi maana ananyenyekea kwa Allaah kwa kumtakasia Yeye nia.

5- Sharti ya tano: Ukweli. Ayaseme maneno haya hali ya kuwa moyo wake unayasadikisha. Akiyasema kwa mdomo wake na moyo wake usiyasadikishe, basi anakuwa ni mnafiki na mwongo. Amesema (Ta´ala):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

“Miongoni mwa watu wako wasemao: “Tumemwamini Allaah na siku ya Mwisho hali ya kuwa si wenye kuamini. [Wanadhani kuwa] wanamhadaa Allaah na wale walioamini lakini hawahadai isipokuwa nafsi zao na wala hawahisi. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah akawazidishia maradhi na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.”[2]

[1] 31:22

[2] 02:08-10

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 19/02/2020