24. Nyoyo zinatakiwa kupewa mazoezi ya mambo ya kheri


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Wanatakiwa pia kuzinduliwa juu ya alama za dini na mipaka ya Shari´ah ili wazowee na kuleleka juu yake na yale mambo ya dini ambayo nyoyo zao zinapaswa kuyaamini…

MAELEZO

Mfumo sahihi wa dini ni yale ambayo yako kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Kwa sababu zipo dini nyingi. Dini sahihi ni yale ambayo yako kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf wa Ummah huu. Kwa hiyo haya ndio yanatakiwa kupandikizwa ndani ya mioyo yao. Watoto wanatakiwa kuhifadhishwa misingi hii ili wakulie juu yake na wayafuate wakishakuwa wakubwa.

Nyoyo zinatakiwa kupewa mazoezi ya kheri kama ambavo miili inapewa mazoezi mbalimbali kama mfano wa kutembea na mazoezi mengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 25
  • Imechapishwa: 13/07/2021