24. Ni yepi maoni yako kwa wanafunzi wenye kumponda Shaykh Rabiy´ na Shaykh Zayd al-Mdkhaliy?


Swali 24: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kuwa yeye hamtambui Shaykh Zayd al-Madkhaliy na Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy kama wanachuoni na kwamba hachukui kutoka kwao kitu hata kimoja katika elimu. Anasema kuwa yeye anamtambua tu Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz. Unawanasihi nini?

Jibu: Tunamuomba Allaah amwongoze. Shaykh Rabiy´ na Shaykh Zayd al-Madkhaliy wote wawili ni katika wanachuoni wanasihiaji. Ni wajibu kwake kuyatambua hayo na asiwatukane. Kuwatukana wao ni kuitukana Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliyobeba. Hatusemi kuwa wamekingwa na kukosea. Lakini hata hivyo tunasema kuwa mfumo wao ni wa Salafiyyah. Ni wajibu kwa wanafunzi wasome vitabu vyao ili waweze kuitambua haki kupitia vitabu hivyo na vya wengine. Lakini tahadharini na vitabu vya Hizbiyyuun.

Ikiwa unataka kumsikia Shaykh ´Abdul-´Aziyz moja kwa moja muandikie [umuulize] ni yepi maoni yake juu ya fulani na fulani halafu baada ya hapo chukua maoni yake endapo atasema kuwa hawa ni katika wanachuoni Salafiyyuun wazuri na uachane na mtazamo ulokuwa nao. Ikiwa atasema kuwa ni wafisadi na Hizbiyyuun basi endelea kushikamana na msimamo wako. Pamoja na hivyo nina uhakika kuwa atawasifu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017