24. Ni ipi hukumu ya sindano na kutumia vidonge?

Swali 24: Ni ipi hukumu ya kupiga sindano na kutumia vidonge[1]?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba kutumia vidonge kunaharibu swawm. Hakuna mwanachuoni anayesema kinyume.

Kuhusu sindano, inaharibu pia swawm ikiwa inapigwa kwenye mishipa. Sindano kwenye misuli inahitajia kuangaliwa. Lililo salama zaidi ni kuiepuka ikiwa hakuna dharurah ya kufanya hivo.

[1] Kutoka “Fath-ur-Rabb al-Waduud” (1/249).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 39
  • Imechapishwa: 12/06/2017