24. Ni ipi hukumu ya mfungaji kutumia sprei mchana wa Ramadhaan kwa sababu ya maradhi?

Swali 24: Ni ipi hukumu ya mfungaji kutumia sprei mchana wa Ramadhaan kwa sababu ya maradhi ya pumu na mfano wake?

Jibu: Hukumu yake ni kufaa iwapo atalazimika kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… na ilhali ameshakubainishieni yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.”[1]

Jengine ni kwa sababu hilo halifanani na kula na kunywa. Hilo limefanana na kuchota damu kwa sababu ya kipimo au sindano isiyokuwa ya lishe.

[1] 06:119

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 07/05/2019