24. Mwenye busara na udugu


1- Anas bin Maalik amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallaam) alifunga udugu kati ya Salmaan na Abud-Dardaa´ na baina ya ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na as-Sa´b bin Jaththaamah.”

2- Haifai kwa aliye na busara kughafilika na kuunga udugu na ndugu na kuwa nao karibu wakati wa majanga na mabalaa.

3- Muhammad bin Waasiy´ amesema:

“Hakuna kitu kilichobaki katika maisha haya isipokuwa swalah ya mkusanyiko, maisha mepesi na ndugu ambaye mtu anafurahika kwaye.”

4- Aliye na busara hatakiwi kufunga udugu wakati wa kipindi kizito na watu wasiojitolea wakati wa raha na shida. Ndugu wa kuunga naye udugu anaweza kuwa bora kuliko ndugu wa damu. Miongoni mwa mambo yanayochunga udugu bora ni kuangalia yale mambo ambayo yule mwingine anapenda.

5- Mapenzi ya kweli ni yale yasiyomili katika mtu kujinufaisha mwenyewe na wala hayaharibiki endapo mtu hapati kitu. Mapenzi ni amani kama ambavyo chuki na woga.

6- Mwenye busara haungi udugu isipokuwa na yule anayemkhalifu katika matamanio yake na anamsaidia katika maoni yake ya sawa na undani wake unaafikiana na uinje wake. Ndugu bora ni wale wasiojadili. Sifa nzuri ni zile zenye kutoka kwa watu wema. Mtu hawezi kujihisi uzuri na mbaya kama ambavyo asiyekuwa mwaminifu hawezi kupendwa.

7- Ma´mar amesema:

“Nilifika nyumbani kwa Qataadah na nilikuwa na kiu. Chumbani kulikuwa kibakuli kikubwa cha maji. Nikamuuliza kama naweza kunywa maji. Akanambia: “Wewe ni rafiki yetu.”

8- Ayyuub as-Sikhtiyaaniy amesema:

“Kitu kinachonipe pupa zaidi ya kuhiji ni kuwa nitakutana na ndugu ambao siwezi kukutana nao katika msimu mwingine zaidi ya huu.”

9- Mwenye busara anatakiwa kutambua kuwa malengo ya udugu sio kukutana, kula na kunywa. Miongoni mwa mambo yanayochangia kuchunga udugu ni kutembea vizuri, kuzungumza kwa chini, mtu kutojiona, mtu kuwa mnyenyekevu na kuacha tofauti.

10- Haifai kwa mtu kuwaomba ndugu zake msaada mara nyingi wasije wakaanza kuona kuwa anaudhi. Huenda mama akamwacha mtoto kwa kunyonya kipindi kirefu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 85-88
  • Imechapishwa: 14/02/2018