24. Mke ahifadhi siri za mume wake

Miongoni mwa haki za mume kwa mke wake ni yeye kuhifadhi siri zake na kunyamaza juu ya yale yanayotendeka nyuma ya milango inapofungwa na khaswa yanayohusiana na jimaa. Haifai hata kumweleza mama yake, dada yake wala rafiki yake wa karibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pengine mwanamke akawaeleza wengine anayofanya na mume wake wakati wanapokuwa faragha naye. Pengine mwanaume akawaeleza wengine anayofanya na mke wake wakati wanapokuwa faragha naye. Mwanamke mmoja akasimama na kusema: “Ninaapa kwa Allaah kuwa wanaume na wanawake wote wanafanya hivo.” Hivyo akasema: “Msifanye hivo.” Nisikuelezeni mfano wa hilo? Hili linafanana na Shetani ambaye anapata mwanamke wa kishetani njiani na akaanza kujamiiana naye na huku watu wanashangilia.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watu walio na nafasi mbaya zaidi kwa Allaah siku ya Qiyaamah ni mwanamume mwenye kufanya jimaa na mwanamke wake na yeye akafanya naye kisha mmoja wao akaeneza siri ya mwenzake.”[2]

[1] al-Kharaaitwiy katika ”Masaawiyl-Akhlaaq” (1/430) kwa mnyororo mzuri au unaokaribia kuwa hivo, kama alivosema Shaykh al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (3153). Hadiyth hii imepokelewa kwa njia zingine kwa Abu Daawuud (2176), Ahmad (2/540-541), al-Bayhaqiy (7/14497) na Ibn Abiy Shaybah kwa maana kama hiyo. Kwa ajili hiyo ameisahihisha al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (7/435) na kusema katika ”al-Irwaa’” (7/73) ina nguvu kwa njia zingine.

[2] Muslim (1437).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 39
  • Imechapishwa: 24/03/2017