4- Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu haki ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum):

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanatambua hadhi ya Maswahabah na kwamba wao ni karne bora kwa ushuhuda wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya yale yaliyothibiti kutoka kwake kupitia kwa ´Imraan bin Huswayn:

“Watu bora ni wa karne yangu, kisha wale waliofuatia, kisha wale waliofuatia, kisha wale waliofuatia.”[1]

Maswahabah bila shaka ndio watu bora wa Ummah huu. Lakini wanatofautiana baadhi wana ngazi za juu kuliko wengine. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ

“Halingani sawa miongoni mwenu aliyejitolea kabla ya u shindi [wa ufunguzi wa mi wa Makkah] na akapigana, hao  watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana – na wote Allaah amewaahidi Pepo.”[2]

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ

“Hawawi sawa waumini wanaokaa [nyumbani] wasiokuwa na dharura na Mujaahiduun katika njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao.”[3]

Lakini ni lazima kujua kwamba ngazi na fadhilah hizi kuna uwezekano mmoja katika wao akawa na ngazi kwa njia isiyofungamana na ngazi kwa njia maalum. Kwa msemo mwingine mtu mmoja huyo anaweza kuwa ni mbora kuliko mwingine kwa njia ya ujumla na ya kuachia na akawa na sifa yenye kumfanya bora kuliko wengine.

[1] Muslim (2651) na Muslim (2535).

[2] 57:10

[3] 04:95

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 20/08/2019