Katika “Adhwaa´ Islaamiyyah” nimetaja mifano mingi ya kutosha juu ya tafsiri ya Sayyid Qutwub ya shahaadah kwamba ni ya Bid´ah na kuwa inathibitisha tafsiri ya wanafalsafa. Anafasiri shahaadah ifuatavyo:

1- Hakuna mwenye kuhukumu asiyekuwa Allaah[1].

2- Allaah hana mshirika katika kuumba na kuvumbua[2]. Hii ni katika maana ya uola (Rubuubiyyah) na sio ya uungu (Uluuhiyyah).

3- Mungu ni Yule aliye na utawala na nguvu[3].

4- Sayyid Qutwub amesema:

“Waarabu walikuwa wakijua maana ya “Ilaah” (mungu) na “Laa ilaaha illa Allaah”… Walikuwa wakijua kuwa uungu (Uluuhiyyah) maana yake ni hukumu ya juu (Haakimiyyah ´Ulyaa).”[4]

5- Sayyid Qutwub amesema:

Laa ilaaha illa Allaah kwa mujibu wa waarabu wenye kuelewa lugha yao maana yake ni kwamba hakuna mwenye haki ya kuhukumu isipokuwa Allaah, hakuna Shari´ah isipokuwa yenye kutoka kwa Allaah na kwamba hakuna yeyote mwenye nguvu juu ya yeyote – kwa kuwa nguvu zote ni za Allaah.”[5]

[1] al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah, uk. 182, chapa ya kumi na tatu.

[2] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (5/2707).

[3] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (6/4010).

[4] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (2/1005).

[5] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (2/1006).