24. Matunda ya elimu: kulingania kwa ujuzi

4- Miongoni mwa matunda ya elimu ni ulinganizi sahihi. Ambaye atakuwa na elimu sahihi basi kulingania kwake katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) kutakuwa sahihi. Allaah (´Azza wa Jall) anasema:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah juu ya elimu – mimi na anayenifuata.”” (12:108)

Allaah (´Azza wa Jall) anamwamrisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aseme:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي

“Sema: “Hii ndio njia yangu.”

Ni njia ipi hiyo?

أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah juu ya elimu – mimi na anayenifuata.””

Huu ndio mfumo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ndio mfumo wa kila atayemfuata kwa haki na ukweli. Analingania katika dini ya Allaah kwa yakini na elimu. Atayelingania katika dini ya Allaah kwa yakini na elimu yuko na hadhi ya juu kabisa. Hatofuata hisia na ujinga. Kinyume chake anamfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu amejifunza elimu na kutambua kile alichokuwa akifunza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016