24. Du´aa ya tiba (Ruqyah)


117- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Kundi la Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lilikuwa katika safari wakati walipoikaa kwenye kabila la mwarabu mmoja. Wakaomba wapokelewe kama wageni, lakini wakakataa. Mkuu wa kabila lile akawa amedungwa (na nyoka). Wakajaribu kumtibu kwa kila njia, lakini haikusaidia kitu. Baadhi yao wakasema: “Nendeni kwa lile kundi lililokuja. Huenda wana kitu.” Wakaenda na kusema: “Mkuu wetu amedungwa na nyoka. Tumejaribu kumtibu kwa kila njia, lakini haikusaidia kitu. Je, mna lolote?” Mmoja wao akasema: “Ninaapa kwa Allaah ya kwamba nina tiba, lakini ninaapa kwa Allaah ya kwamba tumewaomba mtupokee kama wageni, lakini mmkakataa. Sintowatibu mpaka mtupe ujira kwa hilo.” Wakakubaliana kundi la kondoo. Akaanza kumtemea cheche za mate na kusoma:

الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Himdi zote ni Zake Allaah, Mola wa walimwengu.” (al-Faatihah 01 : 01)

Mtu yule akawa mchangamfu kana kwamba ameachwa huru kutoka kwenye uenyekiti. Akaanza kutembea na kutohisi maumivu yoyote. Wakawapa ujira ambao walikubaliana. Baadhi yao wakasema: “Ugawiwe.” Wengine wakasema: “Msifanye lolote mpaka mtapofika kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza yaliyopitika, tuangalie atatuamrisha nini.” Wakafika kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza yaliyopitika. Akasema: “Umejua vipi kuwa [Suurah hii] inatibu?” Kisha akasema: “Mmefanya jambo la sawa. Igaweni na mnipe sehemu” na akaanza kucheka.”

118- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaombea kinga al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa kusema:

أُعِيذُكما بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّةِ مِنْ كُل شَيْطَانٍ وَهَامَّةٍ وَمِنْ كُلِّ عَيْنٍ لامَّةٍ

“Ninawakinga kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia awakinge dhidi ya kila Shaytwaan, uvamizi na kila kijicho chenye kudhuru.”

Anasema:

“Namna hii ndivyo baba yenu [Ibraahiym] alivyokuwa akimuombea kinga Ismaa´iyl na Ishaaq.”

119- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) ameeleza kwamba wakati mtu alipokuwa na maumivu, jeraha au donda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya namna hii – Sufyaan bin ´Uyaynah akaweka kidole chake cha shahaadah kwenye ardhi kisha akakipandisha – na kusema:

بسم الله تُرْبَةُ أَرْضِنَا بريقَةِ بَعْضِنَا يُشْفي سَقِيمُنَا بإِذْنِ رَبِّنَا

“Kwa jina la Allaah. Ardhi ya nchi yetu na kwa mate ya mmoja wetu kuwaponya wagonjwa wetu kwa idhini ya Mola Wetu!”

120- Ameeleza pia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaombea kinga watu wa familia yake, akiweka mkono wa kulia juu yao na kusema:

اللهم رب الناس أذهب الباس اشفه وأنت الشافي لا شفاء إلا شفاؤك شفاء لا يغادر سقما

“Ee Allaah! Mola wa walimwengu! Ondoa ugonjwa. Ponya, hakika Wewe tu ndiye Mponyaji. shari Hakuna uponyaji isipokuwa uponyaji wako tu; ponya uponyaji usioacha ugonjwa.”

121- ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw ameeleza kwamba alienda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza kuhusu maumivu anayopata mwilini yanayomsumbua tokea aliposilimu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Weka mkono wako kwenye kiungo chako unapohisi maumivu na sema mara tatu:

بِسْمِ اللهِ

“Kwa jina la Allaah.”

Halafu sema mara saba:

أَعُوذُ بِعِزَّةِ اللهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وأُحَاذِرُ

“Ninaomba kinga kwa Ukuu na Uwezo wa Allaah dhidi ya kila shari (maumivu) ninayopata na ninayotahadharisha nayo.”

122- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayemtembelea mgonjwa ambaye hajafariki na akamwambia mara saba:

أسأل الله العظيم رب العرش العظيم أن يشفيك

“Ninamuomba Allaah, aliye Mtukufu, Mola wa ´Arshiy tukufu, akuponye.”

isipokuwa Allaah Atamponya.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 80-83
  • Imechapishwa: 21/03/2017