24. Du´aa baada ya Tashahhud ya mwisho kabla ya salamu

  Download

55-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ القَـبْر، وَمِـنْ عَذابِ جَهَـنَّم، وَمِـنْ فِتْـنَةِ المَحْـيا وَالمَمـات، وَمِـنْ شَـرِّ فِتْـنَةِ المَسيحِ الدَّجّال

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya kaburi, kutokamana na adhabu ya Jahannam, kutokamana na fitina ya uhai na kifo na kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.”[1]

56-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ القَـبْر، وَأَعـوذُ بِكَ مِـنْ فِتْـنَةِ المْسيحِ الدَّجّـال، وَأَعـوذُ بِكَ مِـنْ فِتْـنَةِ المْحْـيا وَالمْمـات. اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِنَ المْأْثَـمِ وَالمْغْـرَم

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya kaburi, nakuomba ulinzi kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal, nakuomba ulinzi kutokamana na fitina ya uhai na kifo. Ee Allaah! Hakika mimi najikinga Kwako kutokamana na dhambi na deni.”[2]

57-

اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم

”Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi na hakuna asamehaye dhambi isipokuwa Wewe. Hivyo basi, nisamehe msamaha kutoka Kwako na unirehemu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[3]

58-

اللّهُـمَّ اغْـفِرْ لي ما قَدَّمْـتُ وَما أَخَّرْت، وَما أَسْـرَرْتُ وَما أَعْلَـنْت، وَما أَسْـرَفْت، وَما أَنْتَ أَعْـلَمُ بِهِ مِنِّي أَنْتَ المُقَـدِّمُ، وَأَنْتَ المُـؤَخِّـرُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْـت

“Ee Allaah! Nisamehe niliyoyatanguliza, niliyoyachelewesha, niliyoyafanya kwa siri, niliyoyafanya kwa dhahiri, niliyochupa mpaka na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi. Wewe ni mwenye kutanguliza na Wewe ni mwenye kuchelewesha – hapana mungu wa haki mwengine isipokuwa Wewe.”[4]

59-

اللّهُـمَّ أَعِـنِّي عَلـى ذِكْـرِكَ وَشُكْـرِك وَحُسْـنِ عِبـادَتِـك

“Ee Allaah! Nisaidie juu ya kukutaja, kukushukuru na kufanya vyema katika kukuabudu.”[5]

60-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعوذُ بِكَ مِنَ البُخْـل، وَأَعوذُ بِكَ مِنَ الجُـبْن، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلى أَرْذَلِ الـعُمُر، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَـةِ الدُّنْـيا وَعَـذابِ القَـبْر

”Ee Allaah najikinga Kwako kutokamana na ubakhili, najikinga Kwako kutokamana na woga, najikinga Kwako kutokamana na kurudishwa katika umri duni, najikinga Kwako kutokamana na fitina ya dunia na adhabu ya kaburi.”[6]

61-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وأَعوذُ بِـكَ مِـنَ الـنّار

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba Pepo na najilinda Kwako kutokamana na Moto.”[7]

62-

اللّهُـمَّ بِعِلْـمِكَ الغَـيْبِ وَقُـدْرَتِـكَ عَلـى الْخَلقِ, أَحْـيِني ما عَلِـمْتَ الحـياةَ خَـيْراً لـي، وَتَوَفَّـني إِذا عَلِـمْتَ الوَفـاةَ  خَـيْراً  لـي، اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْـأَلُـكَ خَشْيَتَـكَ في الغَـيْبِ وَالشَّهـادَةِ، وَأَسْـأَلُـكَ كَلِمَـةَ الحَـقِّ في الرِّضـا وَالغَضَـب، وَأَسْـأَلُـكَ القَصْدَ في الغِنـى وَالفَقْـر، وَأَسْـأَلُـكَ  نَعـيماً لا يَنْفَـد، وَأَسْـأَلُـكَ قُـرَّةَ عَيْـنٍ لا تَنْـقَطِعْ  وَأَسْـأَلُـكَ الرِّضـا بَعْـدَ القَضـاء، وَأَسْـأَلُـكَ بًـرْدَ الْعَـيْشِ بَعْـدَ الْمَـوْت، وَأَسْـأَلُـكَ لَـذَّةَ النَّظَـرِ إِلـى وَجْـهِكَ وَالشَّـوْقَ إِلـى لِقـائِـك، في غَـيرِ ضَـرّاءَ مُضِـرَّة، وَلا فِتْـنَةٍ مُضـلَّة، اللّهُـمَّ  زَيِّـنّا بِزينَـةِ الإيـمان، وَاجْـعَلنا هُـداةً مُهْـتَدين

”Ee Allaah, kwa elimu Yako ya ghaibu na uwezo Wako juu ya uumbaji, nihuishe ikiwa unajua kuwa uhai ndio bora kwangu na nifishe ikiwa unajua kuwa kufa ndio bora kwangu. Ee Allaah! Nakuomba kukuogopa kwa siri na kwa dhahiri, nakuomba kutamka neno la haki wakati wa furaha na ghadahbu, nakuomba unifanye niwe kati na kati wakati wa utajiri na umasikini, nakuomba neema isiyomalizika, nakuomba kiburudisho cha macho kisichokatika, nakuomba kuridhika baada ya uliyonikadiria, nakuomba maisha mazuri baada ya kufa na nakuomba ladha ya kutazama uso Wako na shauku ya kukutana Nawe, pasi na madhara yanayodhuru au fitina inayopotosha. Ee Allaah! Tupambe kwa pambo la imani na utufanye tuwe waongofu wenye kuongoza.”[8]

63-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ يا اللهُ بِأَنَّـكَ الواحِـدُ الأَحَـد، الصَّـمَدُ الَّـذي لَـمْ يَلِـدْ وَلَمْ يولَدْ، وَلَمْ يَكـنْ لَهُ كُـفُواً أَحَـد، أَنْ تَغْـفِرْ لي ذُنـوبي إِنَّـكَ أَنْـتَ الغَفـورُ الرَّحِّـيم

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba, ee Allaah, kwa vile Wewe ni Mmoja, uliye Pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye, unisamehe dhambi Zangu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[9]

64-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَـمْدُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَـريكَ لَـكَ المَنّـانُ يا بَديـعَ السَّمواتِ وَالأَرْضِ يا ذا الجَلالِ وَالإِكْـرام، يا حَـيُّ يا قَـيّومُ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وَأَعـوذُ بِـكَ مِنَ الـنّار

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba, kwa vile himdi zote njema ni Zako, hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, hali ya kuwa pekee hana mshirika, Mwingi wa kuneemesha. Ee mwanzishi wa mbingu na ardhi, ee Mwenye utukufu na ukarimu, ee Uliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu. Hakika mimi nakuomba Pepo na najikinga Kwako kutokamana na Moto.”[10]

65-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّـي أَشْـهَدُ أَنَّـكَ أنْـتَ اللهُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـت، الأَحَـدُ الصَّـمَدُ الَّـذي لَـمْ يَلِـدْ وَلَمْ يولَـدْ، وَلَمْ يَكـنْ لَهُ كُـفُواً أَحَـد

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba, kwa vile nashuhudia ya kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, hali ya kuwa ni Mmoja, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[11]

[1] al-Bukhaariy (02/102) na Muslim (01/412) na tamko ni lake.

[2] al-Bukhaariy (01/202) na Muslim (01/412).

[3] al-Bukhaariy (08/168) na Muslim (04/2078).

[4] Muslim (01/534).

[5] Abu Daawuud (02/86) na an-Nasaa´iy (03/35). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Abiy Daawuud” (01/284).

[6] al-Bukhaariy (06/35) kwa nambari (2822) na (639).

[7] Abu Daawuud na Ibn Maajah. Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (02/328)-

[8] an-Nasaa´iy (03/54, 55) na Ahmad (03/364). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh an-Nasaa´iy” (01/281).

[9] an-Nasaa´iy na tamko ni lake (03/52), Ahmad (04/338). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh an-Nasaa´iy” (01/281).

[10] Wameipokea watunzi wa “as-Sunan”. Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (02/329).

[11] Abu Daawuud (05/360). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (02/329) na ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/163).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 20/02/2020