24- Ahmad bin Muhammad ad-Daadiy na Ahmad bin Hamdaan wametuhadithia: as-Shaarikiy ametuhadithia: Abuu Ya´laa al-Mawsiliy ametuhadithia: ´Amr bin Muhammad an-Naaqid ametuhadithia: Ibn ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar: Twaawuus ametuhadithia: Nimemsikia Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) akieleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Aadam na Muusaa (´alayhimaas-Swalaatu was-Salaam) walihojiana ambapo Muusaa akamwambia: “Wewe ndiye baba yetu. Ulisababisha khasara kwetu na tukatolewa Peponi.” Aadam akasema: “Muusaa! Allaah (´Azza wa Jall) alikuteua kwa maneno Yake na akakuandikia Tawraat kwa mkono Wake. Je, unanilaumu kwa kitu ambacho Allaah alikuwa tayari ameshanikadiria miaka 40 kabla ya kuniumba?” Aadam akamshinda Muusaa. Aadam akamshinda Muusaa. Aadam akamshinda Muusaa.”[1]

[1] al-Bukhaariy (6614) na Muslim (2652).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 54
  • Imechapishwa: 30/01/2017