24. Dalili juu ya mkono wa Allaah 10

24- Abu Swaalih al-Aswbahaaniy ´Abdur-Rahmaan bin Sa´iyd bin Haaruun ametuhadithia: Abu Mas´uud Ahmad bin al-Furaat ametuhadithia: Zayd bin ´Awf ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

“Kuna mwanamume kutoka katika watu wa Kitabu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Abul-Qaasim! Je, imekufikia kwamba Allaah (´Azza wa Jall) ataziweka mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, viumbe kwenye kidole, miti kwenye kidole na ardhi kwenye kidole?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na Allaah akateremsha:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]

[1] 39:67

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 27/02/2018