al-Quumiy amesema:

“Amesema:

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ

“Je, mnaamrisha watu mema na [ilihali nyinyi wenyewe] mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu?” (02:44)

Abu ´Abdillaah amesema: “Aayah hii imeteremshwa kwa mnasaba wa wapiga visa na wahubiri. Haya ni maoni ya kiongozi wa waumini. Katika kila minbari kunasimama Khatwiyb mfaswaha anayemsemea uongo Allaah, Mtume Wake na Kitabu Chake.”[1]

Aayah hii inawazungumzisha mayahudi. Pamoja na hivyo Baatwiniyyah Raafidhwah wanaigeuza kwa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na khaswa Maswahabah. Kwa sababu uyahudi ndio dini na chimbuko lao.

[1] Tafsiyr al-Qummiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 57
  • Imechapishwa: 19/03/2017