24. Aina ya kwanza ya majina ya haramu

Shari´ah imeharamisha kumpa mtoto majina yafuatayo:

1- Waislamu wameafikiana[1] juu ya uharamu wa majina yote yanayoashiria kuwa mtu ni mja wa mwingine badala ya Allaah (Ta´ala). Haijalishi kitu ikiwa ni jua, mzimu, mtu au kitu kingine. Mfano wa majina hayo ya haramu ni kama ´Abdur-Rasuul, ´Abdun-Nabiy, ´Abdu ´Aliy, ´Abdul-Husayn, ´Abdul-Amiyr likiashiria kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) na ´Abdus-Swaahib likiashiria al-Mahdiy anayesubiriwa. Haya ni majina ya Raafidhwah.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyabadilisha majina yote yaliyo na uja wa asiyekuwa Allaah. Baadhi ya majina hayo ni ´Abdul-´Uzza, ´Abdul-Ka´bah, ´Abdu Shams na ´Abdul-Haarith.

Ndani ya sampuli hii kunaingia vilevile jina kama Ghulaam-ur-Rasuul na Ghulaam Muhammad linaloashiria “mja wa Mtume”.

Kwa mujibu wa maoni sahihi vilevile imekatazwa kuitwa ´Abdul-Muttwalib.

Katika makosa haya kunaingia vilevile majina yenye uja ambayo mtu anafikiria makosa kwamba ni majina ya Allaah (Ta´ala). Mfano wa majina hayo ni ´Abdul-Maqswuud, ´Abdus-Sattaar, ´Abdul-Mawjuud, ´Abdul-Huwa, ´Abdul-Mursil, ´Abdul-Waahid na ´Abdul-Twaalib. Majina haya yana makosa kwa mitazamo miwili:

Wa kwanza: Haijuzu kumwita Allaah (Ta´ala) kwa jina lisilokuwa na dalili katika Qur-aan na Sunnah.

Wa pili: Haijuzu kutoa jina linaloonyesha kuwa uja anafanyiwa Allaah ikiwa Allaah hakujiita nalo Mwenyewe wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Tazama “Maraatib-ul-Ijmaa´”, uk. 154, ya Ibn Hamz na “Majmuu´-ul-Fataawaa” (01/378-379) ya Ibn Taymiyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 18/03/2017