23. Yanayohusiana na Taqliyd na vigawanyo vyake

Taqliyd inakuwa katika sehemu mbili:

1 – Mwenye kufanya Taqliyd awe si msomi. Yeye kama yeye hawezi kuitambua hukumu. Hivyo itamlazimu kufanya Taqliyd. Amesema (Ta´ala):

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Hivyo basi waulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.”[1]

Amwigilize yule atakayempata mwenye elimu na uchaji zaidi. Wakilingana kwake watu wawili basi atamchagua mbora zaidi katika wao.

2 – Mujtahid afikwe na hali ya haraka na asiweze kufanya utafiti. Basi hapo itambidi kuigiliza.

Kuna Taqliyd aina mbili:

1 – Yenye kuenea.

2 – Maalum.

Taqliyd yenye kuenea ni ile ambayo atalazimiana na madhehebu maalum ambapo atachukua ruhusa na maamrisho yake katika mambo yote yanayohusiana na dini yake.

Wanachuoni wametofautiana juu ya Taqliyd. Miongoni mwao wako ambao wameonelea kuwa ni lazima kwa kutofikia kiwango cha ijtihaad kwa wale waliokuja nyuma. Wengine wameonelea kuwa ni haramu kwa sababu kunampelekea mtu kumfuata moja kwa moja mwengine asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Maoni yanayosema kuwa ni lazima kumtii mwengine asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kila amri na katazo lake ni jambo linalokwenda kinyume na maafikiano. Ujuzishwaji wake ndani yake kuna walakini.”

Andiko maalum (الخاص) ni pale atakapochukua maoni maalum katika suala maalum. Hilo linafaa akishindwa kutambua haki kutokana na ijtihaad yake. Ni mamoja ameshindwa kikweli au ameweza kufanya hivo lakini pamoja na ugumu mkubwa.

Mpaka hapa kimemalizika kitabu “Usuwl-us-Sittah”. Tunamuomba Allaah amlipe vyema mtunzi wacho na atukusanye sisi na yeye katika Pepo Yake. Kwani hakika Yeye ni mwingi wa kutoa, mkarimu. Himdi zote njema zinastahikia Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad.

[1] 16:43

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 37
  • Imechapishwa: 28/06/2021