23. Tafsiri ya maneno ya Ibn ´Abbaas


Pili: Tukizingatia dalili zenye kujuzisha kujifunua basi tutaona ambavyo hazina nguvu sawa na zile zenye kukataza. Yanabainika ifuatavyo:

1- Tafsiri ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) inaweza kufasiriwa kwa njia tatu:

Ya kwanza: Inawezekana alisema hivo kabla ya Aayah yenye kuamrisha kujifunika kuteremshwa, kama jinsi nilivyomnukuu karibuni Shaykh-ul-Islaam akisema.

Ya pili: Inawezekana anacholenga ni yale mapambo ambayo ni haramu kuonesha, kama jinsi alivyosema Ibn Kathiyr katika Tafsiyr yake. Kinachosapoti uwezekano huu ni tafsiri yake (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya Aayah:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake [wote] wa Waumini – ya kwamba [nje ya nyumbani] wajiteremshie mavazi yao ya juu; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane [kuwa ni wanawake wa heshima] na wasiudhiwe. Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

“Allaah amewaamrisha wanawake pindi wanapotoka majumbani wafunike nyuso zao kwa mavazi yao ya juu na waoneshe jicho moja tu.”Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

Ya tatu: Lau tutasema kuwa hakumaanisha si cha kwanza wala cha pili, tafsiri yake si hoja ikiwa Swahabah mwingine anasema kitu kingine. Ikiwa Swahabah mwingine ana kauli nyingine, basi mtu anachukua ile kauli ambayo dalili yake ina nguvu. Katika hali hii Ibn Mas´uud ana kauli nyingine kuliko Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Ibn Mas´uud amefasiri Kauli ya Allaah (Ta´ala):

إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا

“… isipokuwa yale yanayodhihirika…”

na kusema kuwa makusudio ni yale mavazi ya juu ambayo hakuna namna ya kuyaficha. Kwa hiyo ni wajibu kutafuta kauli yenye nguvu na kuitendea kazi.

[1] 33:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 26/03/2017