Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

18- Kama ambavyo siku zote alikuwa ni mwenye kusifiwa kwa sifa Zake, vivyo hivyo ndivo atavoendelea kuwa milele.

MAELEZO

Kama ambavo sifa Zake (Subhaanah) hazina mwanzo kadhalika hazina mwisho. Sifa Zake ni za milele hazina mwisho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wewe ndiye wa Kwanza; hakuna kabla yako kitu. Wewe ndiye wa Mwisho; hakuna baada yako kitu.”[1]

Haya ni kuhusu majina na sifa Zake. Sifa Zake hazitokatika katika mustakabali, kwa sababu ni zenye kuandamana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] Muslim (2713).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 43
  • Imechapishwa: 17/09/2019