23. Sifa na majina ya Allaah yaliyothibiti katika Qur-aan V

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ

Na miongoni mwa watu wako waaowafanya badala ya Allaah kuwa ni mungu mshirika; wanawapenda kama mapenzi [yapasavyo] ya kumpenda Allaah.” (02:165)

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖوَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا

”Na sema: “Sifa njema zote ni za Allaah Ambaye Hakujifanyia mwana, na wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na wala hakuwa dhaifu hata awe [ahitaji] msaidizi; basi mtukuze matukuzo makubwa kabisa.” (17:111)

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Vinamtakasa Allaah [vyote] vilivyomo mbinguni na [vyote] vilivyomo ardhini – ufalme ni Wake na Sifa njema ni Zake – Naye juu ya kila kitu ni Muweza.” (64:01)

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًاالَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

”Ametukuka kwa Baraka Yule Ambaye Ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe muonyaji kwa walimwengu. Ambaye ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, na hakujichukulia mtoto na wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na Ameumba kila kitu; kisha Akakikadiria kipimo sawa sawa.” (25:01-02)

مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

 

”Allaah Hakuchukua mtoto yeyote na wala hakukuwa pamoja Naye mungu mwengine – hapo bila shaka kila mungu angelichukua vile alivyoviumba, na bila shaka baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Ametakasika Allaah kutokana na yale yote wanayoyaelezea. Ni Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri. Basi Ametukuka kutokana na yale wanayomshirikisha.” (23:91-92)

 

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

 
”Basi msipigie mifano Allaah – Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.” (16:74)  
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

”Sema: “Hakika Mola wangu Ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyo ya siri, na dhambi, ukandamizaji bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa chochote kile ambayo Hakukiteremshia dalili, na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui”.” (07:33)

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

Mwingi wa Rahmah amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Kisha Akalingana juu ya ‘Arshi.” (07:54)

Aayah zimekuja kwa sampuli hii mahali saba: al-A´raaf:54, Yuunus:03, ar-Ra´d:02, al-Furqaan:59, as-Sajdah:04 na al-Hadiyd:04.

MAELEZO

Aayah zote hizi ni zenye kubainisha baadhi ya sifa za Allaah (´Azza wa Jall) kama zile zilizotangulia. Mfumo wa Ahl-us-Sunnah kwazo inatakiwa kuziamini na kuzithibitisha kama zilivyokuja kwa njia inayolingana na Allaah. Inatakiwa kufanya hivyo pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kuzifananisha.

Hali kadhalika inahusiana na zile sifa za Allaah zilizokuja katika Sunnah Swahiyh. Zote ni kwa mfumo huu: ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia inayolingana na Allaah pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kuzifananisha. Miongoni mwazo ni maneno Yake (Jalla wa ´Alaa):

Dalili ya Allaah kutokuwa na wenza na washirika

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا

Na miongoni mwa watu wako waaowafanya badala ya Allaah kuwa ni mungu mshirika.” (02:165)

Bi maana wenza na washirika. Allaah hana wenza wala washirika. Amesema:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا

Na miongoni mwa watu wako waaowafanya badala ya Allaah kuwa ni mungu mshirika.”

kwa njia ya makemeo. Kwa msemo mwingine kuna watu wenye kumfanyia Allaah washirika. Nao si wengine ni washirikina. Ndipo akakataza hili pale aliposema:

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)

Bi maana msiwaabudu walioko ndani ya makaburi, Mitume, Malaika, majini na mawe. Vyote hivyo kuviabudu ni batili. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Kweli na wale wanaowaomba badala Yake ndiyo batili.” (22:62)

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الْبَاطِلُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Kweli na wale wanaowaomba badala Yake ni batili.” (31:30)

Ni wajibu kwa kila kiumbe ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia kumuabudu Yeye Mmoja wa Pekee na wawakanushe wenza. Wanatakiwa kutambua kwa yakini ya kwamba hana mwenza, mwenye kulinhgana Naye na mshirika na wakati huo huo waamini hilo. Amesema (Ta´ala):

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na wala hana yeyote anayefanana [kulingana] Naye.”(112:03-04)

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

 
”Basi msipigie mifano Allaah! Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.”(16:74)  

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

Amesema (Ta´ala):

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖوَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا


”Na sema: “Sifa njema zote ni za Allaah Ambaye Hakujifanyia mwana, na wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na wala hakuwa dhaifu hata awe [ahitaji] msaidizi; basi mtukuze matukuzo makubwa kabisa.”
(17:111)

Allaah hana mshirika katika ufalme. Allaah ana mawalii. Lakini hata hivyo sio wasaidizi katika ufalme Wake. Yeye ni Mwenye kujitosheleza na kila asiyekuwa Yeye. Yeye ndiye Mwenye nguvu, Aliye juu na Mshindi. Hana washirika katika ufalme. Pamoja na hivyo ana mawalii Anaowapenda na wao wanampenda. Yule mwenye kumtii na kumcha ndio walii Wake kwa njia ya kwamba Allaah anakuwa ni mwenye kuwapenda na kuwakaribia, kwa sababu wamemtii na kuadhimisha maamrisho Yake. Amesema (Ta´ala):

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.” (10:62:63)

Hawa ndio mawalii wa Allaah. Lakini hata hivyo sio wasaidizi katika ufalme. Ni mawalii kwa njia ya mapenzi, kwa sababu wamemtii na kufuata Shari´ah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Vilevile inahusiana na Aayah nyenginezo zenye kutaja ufalme, sifa kamilifu na uwezo. Hakika Yeye ndiye Mfalme juu ya kila kitu, Muumbaji wa kila kitu, Muweza juu ya kila kitu na ni Mjuzi wa hali zote za waja. Yote haya ni haki. Miongozi mwazo ni pamoja na:

Dalili ya Allaah kutokuwa na mtoto

وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا

“… na hakujichukulia mtoto.” (25:02)
 

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

 
  “Na wala hana yeyote anayefanana [kulingana] Naye.” (112:04)  

Sifa zote hizi ni zimethibiti Kwake (Jalla wa ´Alaa). Yeye ndiye Muumbaji wa kila kitu:

Dalili ya Kuumba na Uwezo wa Allaah

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

“… na Ameumba kila kitu; kisha Akakikadiria kipimo sawa sawa.” (25:02)

لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“… ufalme ni Wake na Sifa njema ni Zake. Naye juu ya kila kitu ni Muweza.”(64:01)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com