23. Shirki ndio dhambi kubwa mno ambayo kaasiwa Allaah

Shirki ndio dhambi kubwa mno. Dhambi kubwa ambayo Allaah kaasiwa kwayo ni shirki. Kwa ajili hii ndio maana ameitaja kuwa haramisho la kwanza.  Amesema (Ta´ala):

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

”Sema: “Njooni nikusomeeni yale aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu kwamba: Msimshirikishe na chochote.” (al-An´aam 06:151)

Amesema vilevile:

لَّا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا

”Usifanye pamoja na Allaah mungu mwengine, ukaja kusemwa vibaya na mwenye kutupiliwa mbali.” (al-Israa´ 17:22)

وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا

”Na wala usifanye pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja kutupwa katika Moto hali ya kuwa mwenye kulaumiwa na kufukuziliwa mbali.” (al-Isaa´ 17:39)

فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ

“Basi usiombe pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa.” (ash-Shu´araa´ 26:213)

Haijuzu kumfanya pamoja na Allaah mwengine katika ´ibaadah. Kwa sababu ´ibaadah ni haki ya kipekee anayofanyiwa Allaah (´Azza wa Jall). Haiistahiki yeyote kinyume na Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 42
  • Imechapishwa: 04/07/2018